This archive report was first published on 21 September 2019.
Wabunge wa Jubilee Washinikiza Chama Kumuua Muasi Maina Kamanda ¶
Mnamo Alhamisi, Septemba 19, 2019, Maina Kamanda alitangaza hadharani kwamba anamuunga mkono Imran Okoth ambaye ni mgombea wa ubunge Kibra chini ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM) licha ya Jubilee kuwa na mgombea McDonald Mariga.
Wanasiasa wa chama tawala cha Jubilee wamezua tetesi wakishinikiza kutimuliwa kwa Kamanda kwa kile walichokitaja kama kuwa ukaidi.
Wakati wa hafla ya iliyoandaliwa na wanawake wa vuguvugu la Inua Mama Jenga Taifa, mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kirinyaga Purity Ngirichi alisema Kamanda anaenda kinyume na maadili ya Jubilee licha ya kupewa kiti na chama hicho.
Ngirichi alisema iwapo Kamanda hataadhibiwa basi wanasiasa wengine watafuata mkondo huo na kumkaidi rais Uhuru Kenyatta.
"Amesema ataunga mkono mgombea wa ODM kule Kibra, ilhali (Jubilee) tulimpa kiti bure wala hakupigania. Iwapo ni hivyo, basi ajiuzulu na kujiunga na chama hicho apewe kiti huko. Wadhifa wake utapewa viongozi wengine ambao wanastahili," alisema Ijumaa 20, Septemba kaunti ya Taita Taveta.
Matamishi hayo ni sawia na yale ya mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa ambaye alisisitiza ni sharti adhabu itolewe kwa wale ambao hawamuungi mkono Mariga.
"Wanachama wa Jubilee ambao wanaenda kinyume na maadili ya chama wanapaswa kuchukuliwa hatua kali kwa kuwa waasi," Barasa alisema.
Awali kulingana na The Standard, katibu wa Jubilee Raphael Tuju alisema kuwa anafanya mashauriano na kamati nzima ya chama hicho ili kuafikiana ni hatua ipi Kamanda atachukuliwa kwa kumuunga mkono Okoth licha ya kuwepo kwa Mariga wa Jubilee kwenye kinyang'anyiro hicho.