This archive report was first published on 20 September 2019.
September 20, 2019 - Mmiliki wa hoteli moja mjini Kericho alichemka baada ya kumpata weita aliyejiuzulu akipakua chakula jikoni ilhali alikuwa sio mfanyikazi wake tena.
Alitaka nyongeza ya mshahara lakini wakati alijaribu kumkumbusha mwajiri wake, alimtaka ajiuzulu iwapo ameshindwa na kazi.
Alijiuzulu mara moja na akaanza kutangatanga mjini akisaka kazi kwingine.
Alilazimika kurejea mkahawani akiwa na njaa na kujipakulia ugali mlima na kitoweo cha bwerere kama alivyozoea akifanya kazi hapo.
Alitia sikio nta wakati weita mmoja alimshauri kwamba angekiona cha mtema kuni iwapo angepatikana.
Alishtuka nursa aangushe sahani ya mlo sakafuni wakati mdosi aliingia na kumkodolea macho.