Skip to main content

Gavana Sonko Amlipia Karo Mvulana Aliyekuwa Akitambaa Kwenda Shuleni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 September 2019.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amempa msaada mvulana wa darasa la nne kutoka shule ya msingi ya Aderema Price School eneo la Amukura, kaunti ya Busia ambaye amekuwa akitambaa hadi shuleni kwa miaka sita.

Alisema mwanafunzi huyo alitembelewa na Sonko Rescue Team ambao walimpa zawadi na chakula kabla ya kumsajili katika shule hiyo.

Alisajili mwanafunzi huyo kwa shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na kumilipia karo yake kando na kumnunulia bidhaa muhimu za matumizi shuleni.

Wakati wa kujisalimisha kwenye shule hiyo, Sonko alisema, "Leo, kundi la Sonko rescue team lilimtembelea huko kaunti ya Busia, kumsajili katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, akapokea kiti cha magurudumu na bidhaa za mahitaji yake shuleni."

Ukarimu wa Sonko ulikuwa wa kipekee, kwani baadhi ya Wakenya vile vile walijitokeza na kununua viti vya magurudumu ambavyo kulingana na msimamizi wa mradi huo vilipewa watu wengine wenye ulemavu.

Wakati huo huo, viongozi wengine walitoa msaada, pamoja na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Busia Florence Mutua na mbunge mteule David Ole Sankok.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →