Skip to main content

Mbunge wa Mugirango Kusini Amtaka Imran Okoth Kuingia Mashinani Kusaka Kura

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 September 2019.

Uchaguzi wa Kibra utakuwa wa ushindi kwa mgombea ambaye ataingia kwa wapiga kura na kujipigia debe vilivyo, kwa kauli ya Mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro.

Osoro alisema hilo baada ya Imran Okoth, mgombea wa ODM, kufanya mkutano na wananchama wa ODM kutoka Kibra.

Imran Okoth anatarajiwa kumenyana na wagombea wa Jubilee na ANC kwenye uchaguzi huo mdogo utaofanyika Novemba 7.

Imran tayari anaungwa mkono na kinara wa ODM Raila Odinga pamoja na viongozi wa Jubilee kama vile Maina Kamanda.

Osoro alizungumza siku moja tu baada ya Imran kufanya mkutano na wananchama wa ODM kutoka Kibra.

Osoro alisema, "Mimi si mpiga kura Kibra na sina wafuasi huko. Siko Jubilee, ANC wala ODM lakini Iran ni rika yangu na ninataka kumwambia jambo moja. Kama ningalikua yeye, ningeingia mashinani. Buda, toka kwa hizi mikutano za wanahabari na uchape ground," alisema Osoro.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →