This archive report was first published on 18 September 2019.
Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amesherekea kukataliwa kwa mswada wa Punguza Mzigo ambao ulipitishwa na Kaunti ya Murang'a Jumanne, Septemba 17, 2019.
Waiguru alisema eneo la Mlima Kenya haliungi mkono Punguza Mzigo, huku akiwakejeli wafuasi wa Tangatanga kwa kushindwa kusaka kura za kupitisha mswada huo.
"Eneo la Mlima Kenya linaongea kwa sauti moja dhidi ya mswada wa Punguza Mzigo.....na kwa sasa viongozi waliokuwa wakiunga mkono wamegeuka," alisema Waiguru.
Waiguru amekuwa akiendesha kampeni kupinga mswada huo wa Aukot, huku Kaunti yake ikiukataa mnamo Septemba 10, 2019.
Alisema pia anataka Wakenya kusubiri mapendekezo ya BBI ili kujua mwelekeo watakaochukua.