This archive report was first published on 17 September 2019.
Victor Kinuthia, mwanahabari wa runinga na redio ya Inooro, amejitosa kwenye nyanja ya muziki baada ya kubabaishwa na wakenya kwa kuzungumza Kizungu kibovu wakati alipokuwa akiripoti.
Alipata muda wa kuripoti runinga ya Citizen kwa Kizungu, alikuwa na wakati mgumu, na hivyo alitumia muda huo kuingia studioni na kurekodi wimbo ambayo inazungumzia suala hilo.
Wimbo huo, ulioitwa Kirindi, uliwekwa kwenye YouTube siku ya Jumamosi, Septemba 14, na tayari imewavutia watu 11,000.
Wimbo huo unamaanisha kutawazwa katika lugha ya Kikuyu, na Kinuthia anajaribu kuwahimiza watu kuwapuuza wanaowakashifu lakini kumuegemea Mwenyezi Mungu.
Alitumia kisa hicho kwenye mstari wa kwanza wa wimbo wake, jambo ambalo ni njia ya kuwapuuza watesi wake.
Alipokuwa amekabithiwa jukumu la kuripoti mubashara kwa lugha ya Kizungu wakati Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro alikamatwa Muranga siku ya Jumatatu, Septemba 9, wakenya walimshambulia mtandaoni kwa kutoridhishwa na kuripoti kwake.