Skip to main content

KRA Nasa Mwanamke Akisafirisha Stempu Feki Kutoka China

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 14 September 2019.

Maafisa wa KRA walikamatwa mwanamke mmoja akiwa JKIA, ambaye alishukiwa kuwa na stempu feki za KRA kutoka China.

Alitambulika kama Jane Mary Muthoni Gichengo, aliyenaswa pindi tu alipowasili kutoka China. KRA iliongeza kwamba Gichengo alikuwa mmoja wa genge linalounda stempu nchini China na kisha kuzisafirisha hadi Kenya.

Stempu hizo zinasambazwa kupitia wahusika wengine wa genge hilo ambao wanawauzia wamiliki wa viwanda vya kuuza pombe na hivyo basi kupotea kwa pesa za ushuru.

Alisubiri kufikishwa mahakamani baada ya KRA kudokeza kwamba itakaza kamba kupigana na bidhaa za magendo zinazosambaa sokoni kwa minajili ya kuziba mianya ya ukwepaji ushuru.

Maafisa wa KRA waliharibu bidhaa za magendo zenye thamanani ya takriban KSh 1.5 milioni, ambazo zilinaswa kutoka kwa wafanyabiashara jijini Nairobi na viunga vyake.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →