This archive report was first published on 13 September 2019.
Wakili Ahmednasir Abdullahi amedai kwamba ndoa ya kisiasa kati ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ina mitazamo miwili.
Wakili huyo amesema kwamba ndoa hiyo tayari ilikuwa imefikia kikomo, lakini kisheria inapaswa kuwa hai.
Alisema hivi kwa ujumbe aliouchapisha Ijumaa, Septemba 13 kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Alidai kwamba ukweli ni kwamba ndoa hiyo tayari ilikuwa imefikia kikomo, lakini kisheria inapaswa kuwa hai.
Aliongeza kwamba ni bayana kwamba upendo uliokuwepo kati ya waili hawa haupo tena.
Alisema kwamba tatizo hili lilisabishwa na siasa za urithi.