This archive report was first published on 12 September 2019.
Caster Semenya atatuzwa Rasmi Medali ya Dhahabu ya Mwaka 2011 ¶
Wanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya atatuzwa rasmi medali yake ya dhahabu ya mwaka 2011 wakati wa mashindano ya mwaka huu yatakayoandaliwa mjini Doha, lakini hatakuwepo kuipokea.
Medali hiyo ilikuwa iliyotarajiwa sana kwa Semenya, ambaye alikuwa na hamu ya kutetea taji lake la mwaka 2017 mjini Doha, mnamo mwezi Septemba 27, lakini alilazimika kujiondoa kwenye mashindano hayo huku bado mahakama ya Uswizi haijatoa uamuzi wake katika kesi ya kushiriki mashindano bila kutumia dawa za kupunguza homoni za kiume mwilini mwake.
Shirika la Riadha nchini Afrika Kusini (ASA), lilithibitisha siku ya Alhamisi kuwa Semenya hatajiwasilisha mjini Doha, kupokea medali yake binafsi wakati wa sherehe ya IAAF, lakini kutakuwa na atakayemwakilisha.
“Hongera kwa wanariadha wetu kwa hatua waliopiga na kwa kutambuliwa kama wanariadha wasafi,” alisema rais wa ASA, Aleck Skhosana kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.
“Tunafuraha kuwa IAAF sasa imewapa nafasi washindi wanaostahili kuwa katika sherehe hiyo ambapo waliopotoka walinyimwa,”aliongezea rais huyo.
Wanariadha wengine walio na utofuati wa ukuwaji wa kijinsia (DSDs), walipigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya IAAF baada ya kukiuka sheria za dawa za kusisimua misuli.
“Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected].