This archive report was first published on 10 September 2019.
Wanahabari wengi wamekumbwa na taarifa zao zikisambaa kwenye mitandao, na baadhi yao wamekata tamaa katika mambo wanayofanya.
Victor Kinuthia, mwanahabari wa Inooro TV, alikuwa na uzoefu huo Jumanne, Septemba 10, 2019, baada ya kufanya uanahabari Jumatatu, Septemba 9, 2019.
Alisema alikuwa amefikiria kuwacha uanahabari baada ya kupata taarifa yake kwa mtandaoni, lakini wadosi wake na marafiki wakampa moyo kuendelea.
"Karibu ni kate tamaa kwenye uanahabari baada ya kupata nimesambaa kwenye mtandao kutokana na taarifa yangu ya saa tatu jana. Lakini baada ya kupata jumbe kutoka kwa wadosi wangu na marafiki, wamenitia moyo," alisema Kinuthia.
Wanahabari waliobobea wakiongozwa na Joe Ageyo, Hussen Muhammed na Francis Gachuri waliwataka Wakenya kuwa wapole kwa Kinuthia kwani si kazi rahisi kuenda hewani.