This archive report was first published on 9 September 2019.
Published on September 9, 2019, Mbunge wa Gatundu Moses Kuria amewashutumu vikali baadhi ya wanasiasa katika Chama cha Jubilee kwa kutatiza amani katika kanisa la Gitui, Murang'a, Jumapili, Septemba 8, 2019.
Alisema tabia ya wanasiasa kutovumiliana eneo la Mlima Kenya haiwezi kuruhusiwa kuendelea kama inavyofanyika sasa.
Alisema hilo kupitia ujumbe wake wa Facebook, ambapo alishangazwa na kampeni za mapema za wanasiasa katika Mlima Kenya na kupigania viongozi ambao huenda baadaye wakaungana kufanya kazi pamoja 2022.
Alisema, "ODM ilifanya uteuzi Kibra bila ya vita. Lakini katika Jubilee Kieleweke na Jubilee Tanga Tanga walikosa heshima katika Nyumba ya Mungu huko Muranga. Huku tukingani na zaidi ya siku 1,000 kaba ya uchaguzi ujao. Pande zingine za nchi ni tulivu," alisema.
Aliongoza kwa kusema, "Unaweza kudhani uchaguzi ujao utafanyika Mlima Kenya pekee. Utaambia nini watu wakati Raila Odinga na William Ruto wakiungana kuchukua 2022?"
Alisema hilo kwa kuashiria kwamba Jubilee lazima iwe na akili katika uchaguzi wa 2022.