Skip to main content

Mbunge Ngunjiri Wambugu Afichua Kuwa Ruto Huwahonga Wanasiasa Kuhudhuria Hafla Zake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 8 September 2019.

Naibu Rais William Ruto Akikashifuwa na Mbunge wa Nyeri Mjini

Naibu Rais William Ruto amekashifuwa na mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu kwa kuwahonga viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya ili kumuunga mkono kwenye azma yake ya kuwania urais 2022.

Wambugu alidai kuwa baadhi ya wabunge kutoka mkoa wa Kati wa Kenya hupokea hongo kufanya ziara na DP Ruto kote nchini kila Ijumaa na Jumamosi.

Alidai kuwa pesa ndizo zinawachangia wabunge hao kumuunga mkono Ruto katika azma yake ya kuwania urais 2022.

Wambugu anasisitiza kuwa sababu ya wabunge hao kukubali kuandamana na Ruto kote nchini kumfanyia kampeni ya 2022, ni pesa.

Alisema, "Mbona nisafiri kote nchini kumpigia debe mgombeaji wa urais kama silipwi...na hakuna uchaguzi? Lazima wanatiwa motisha na pesa..Hauwezi kuniambia kuwa unatembea kote nchini huku umeacha eneo bunge lako kila siku ya Ijumaa na Jumamosi kumpigia debe mtu ambaye atawania urais kwa kipindi cha miaka mitatu..kwa sababu unampenda?"

Wambugu amekuwa akipinga vikali Ruto kisiasa eneo katika hilo huku majuzi akitangaza kuwa eneo bunge lake sio mahala pa kufanyia kampeni za 2022.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →