Skip to main content

Maureen Kunga, Mwanamuziki wa Kundi la Elani, Ameunga Ndoo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 6 September 2019.

Maureen Kunga, mwanamuziki wa kundi la Elani, amefunga ndoa katika harusi ya kufana kando ya ziwa la Naivasha mwishoni mwa Agosti.

Harusi hiyo iliyohudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wake wa karibu iliyofanyika kwa usiri mkubwa.

Maureen aliwajuza mashabiki wake kuhusu harusi yake kwenye picha aliyoipakia katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amevalia gauni la harusi na veli.

Harusi hiyo imeandaliwa miezi michache tu baada ya mwanamuziki huyo kufunga ndoa ya kitamaduni kwenye sherehe iliyofanyika Disemba 9, 2018.

Maureen Kunga akijivinjari katika densi wakati wa sherehe ya harusi yake.

Wambui, mwanamuziki mwenza ambaye pia yuko katika kundi la Elani alikuwa mmoja wa maarusi wa kike kulingana na picha ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni.

Wageni waalikwa walipata fursa ya kulisha macho kwa mandhari ya kupendeza ya Ziwa la Naivasha kuhudhuria harusi ya Maureen Kunga.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →