This archive report was first published on 6 September 2019.
Polisi wamepata masanduku yaliyokuwa na shilingi milioni 72 zilizoibiwa kama yametupwa kwenye msitu Kaunti ya Kiambu.
Wakati huo huo, simu ya rununu pia ilipatikana katika eneo ambapo masanduku hayo yalikuwa yametupwa.
Polisi Kaunti ya Kiambu walisema masanduku hayo yalipatikana baada ya mkazi mmoja kuyaona na kufahamisha maafisa wa polisi.
Wafanyikazi wa kampuni ya G4S walikuwa wakizipeleka kwenye ATM za mabenki jijini Nairobi wakati waliokuwa wamevalia sare za polisi walitokea na kuwazubaisha kabla ya kutoweka na fedha hizo zote.
Wakenya kwenye mitandao walitaja wizi huo kama 'sinema kama vindio'.
Polisi wangali wanachunguza kisa hicho.