This archive report was first published on 5 September 2019.
Polisi wa Kenya wamekamatwa raia mmoja wa Nigeria na mwenzake kutoka Congo kwa kupatikana na noti feki za KSh. 1k. Mnamo Septemba 3, 2019, wawili hao waliopatikana wakiwa na noti feki za KSh. 1k. walikamatwa katika kijiji cha Kakumini, Kaunti ndogo ya Yatta.
Washukiwa hao, Ogundeji Olayinka na Tazisong Fabian, walikamatwa na hatimaye kufikishwa kortini mnamo Alhamisi, Septemba 5.
Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka nyumbza za washukiwa kupigwa sachi na ombi lake kuruhusiwa.
Stakabadhi za kortini zilisema, "Mnamo Septemba 3, 2019, kwa kushirikiana walipatikana wakiwa na noti feki za Ksh. 1000 zenye nambari za usajili AA0209039 (noti mbili), AA0209229 (noti mbili), AA0209033 (noti tatu) na AA0229042 (noti mbili)".
Sehemu ya 359 ya Sheria za Kenya kuhusu vitendo vya aina hiyo inasema kuwa, yeyote anayepatikana na kosa la aina hiyo anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka saba jela.