This archive report was first published on 3 September 2019.
Alama mbaya ya uroda ilionekana baada ya kalameni kuporwa kitita cha KSh 10,000 na mwanadada akiyemchota mtaani.
Penyenye zinasema kwamba, baada ya wawili hao kulishana mahaba kipusa, kalameni aliomba kuenda msalani lakini hakurejea chumbani.
Alipomtafuta kipusa, aligundua kuwa mwenzake tayari alikuwa ametoweka baada ya kumpora hela zake zote.
Landilodi alimkuta kalameni akinuna kwa mahangaiko na baada ya kumhoji aligundu alikuwa amepoteza hela.
"Wewe nakujua vizuri. Una mke na watoto nyumbani. Umekuwa ukinyemelea vipusa mtaani na sasa wamekutenda," landilodi alimwambia kalameni.