Skip to main content

Huenda Victor Wanyama Akarejea Celtic Kwa Mkataba wa Mkopo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 2 September 2019.

Victor Wanyama, mchezaji wa zamani wa Southampton, anahusishwa na kurejea katika klabu ya Scotland ya Celtic kwa mkataba wa mkopo. Hii ni baada ya kurejea kwenye orodha ya wachezaji wa Tottenham chini ya uongozi wa Mauricio Pochettino.

Wanyama aliondoka Celtic mwaka 2013 akijiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Southampton. Sasa, tayari Tottenham wako huru kumruhusu kiranja wa Harambee Stars kurejea Parkhead.

Spurs wanasemekana kuwa makini kuwasilisha ofa ya mkataba wa mkopo kwa sogora huyo wa zamani wa Southampton endapo watashindwa kumsajili kwa mkataba wa kudumu kabla mchakato wa uhamisho wa bara Ulaya kukunja jamvi.

Neil Lennon, meneja wa Celtic, anaaminika kuwa makini kuzipata huduma za Wanyama baada ya kuwa na wakati nzuri na mchezaji huyo awali.

Wanyama alichezea Celtic kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Southampton mwaka 2013.

Source: UGC

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →