This archive report was first published on 1 September 2019.
Mwanamke Mwenye Matumaini: Pam Talbert Ateuliwa Naibu wa Mwalimu Mkuu Baada ya Kuhudumu kama Msafishaji ¶
Published on September 1, 2019
Pam Talbert, ambaye kwa wakati moja alikuwa akihudumu kama msafishaji shuleni, alikuwa mwenye bidii ya muchwa na mvumilivu ili kufikia kilele cha taaluma yake kama naibu wa mwalimu mkuu.
Alipokuwa na ulemavu wa kusoma, watoto wake walimsaidia kwenye ufanisi wake na kumlazimu kutoka kwenye starehe zake. Kila wanawe walipokuwa wakirejea kutoka shuleni, walikuwa wakimfunza mama yao.
Naibu huyo wa mwalimu mkuu mwenye bidii, alikuwa akijifunza kupitia kwa kile watoto wake walikuwa wakisoma shuleni. Hatimaye, aliweza kurejea shuleni na kufuzu na shahada ya mbili ikiwemo ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Southern.
"Miujiza hufanyika kama unatafuta miujiza. Mimi ni miujiza. Sikuwa na uwezo wa kuandika wala kusoma. Nilikuwa katika darasa la tatu," alisema mama huyo.
"Licha ya kule unatoka, historia yako ama pale unaishi...mambo yatakuwa sawa endapo utavumilia ikiwa utajaribu," Talbert alisema.
Jambo la kufarahisha zaidi, Pam na mwanawe wa kiume wanapania kusomea shahada zao za uzamifu katika Chuo cha Southern University.