Skip to main content

Msanii wa Nyimbo za Injili Audrey Chibole Afariki Baada ya Kuugua Saratani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 31 August 2019.

Msanii wa nyimbo za injili Audrey Chibole, ambaye alijulikana kama Audrianna, amefariki baada ya kuugua saratani ya maini.

Alifariki akiwa na umri wa miaka 22, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamake.

Alisoma muziki na kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, na alikuwa ni mwanafunzi katika chuo hicho.

Alianza kuteta kuhusu maumivu kwenye viungo vya mwili wiki mbili zilizopita na akafikishwa katika hospitali ya rufaa ya Kakamega ambapo alipata matibabu.

Aligunduliwa kuwa na saratani ya maini baada ya kusafirishwa mpaka hospitali ya Nairobi.

Wasanii mbali mbali wamekuwa wakituma rambirambi zao kwa familia kutokana na kifo cha nyota huyo.

Alifariki Jumanne, Agosti 27, alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.

Alionekana kuwa ni msanii chipukizi ambaye alijulikana kwa wimbo wake wa Niko Sawa ambapo alimshirikisha mwanawe mwanahabari Ann Ngugi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →