Skip to main content

Neymar: Barcelona na PSG Washindwa Kuafikiana kuhusu Thamani ya Raia Huyo wa Brazil

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 30 August 2019.

Paris Saint-Germain ya Ufaransa imeendelea kufanya mambo kuwa magumu kwa staa wake Neymar kuondoka baada ya kukataa ofa ya Barcelona kwa mara nyingine.

Na huku dirisha la usajili Ulaya likitarajiwa kufungwa Jumatatu, Septemba 2, Barcelona wanafanya kazi kubwa wakitarajia kumrejesha raia huyo wa Brazil katika timu yao.

PSG wanaamini ofa hiyo inatosha baada ya kuwa wagumu kuikubali mwanzoni na hii ni licha ya mchezaji mwenyewe kuonyesha nia ya wazi ya kutaka kuondoka klabuni hapo.

Wakati PSG wanaamini ofa hiyo inatosha, Barcelona wanataka zaidi ya pauni 198 milioni ambacho PSG ilikitoa ili kumsajili Neymar miaka miwili iliyopita kutoka Barcelona.

Wakati huohuo, kuna madai kuwa wapinzani wa jadi wa Barcelona, Real Madrid wapo kwenye mazungumzo mazuri ya kufanikiwa kumsajili mchezaji huyo.

Itakumbukwa kuwa, Neymar hajaichezea PSG tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kuandamwa na majeraha ya kifundo cha mguu ambayo yalisababisha pia akakosa michuano ya Copa America 2019.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →