This archive report was first published on 30 August 2019.
Maafisa wa polisi waliokamatwa na CCTV wakiiba pesa na simu kutoka duka la M-Pesa katika mtaa wa Kasarani, Nairobi, Jumamosi, Agosti 24.
Wanjiru Karikui, mfanyabiashara wa duka hilo, anawalaumu polisi ambao waliondoka na kiasi kisichojulikana cha pesa kutoka kwa duka lake la M-Pesa na baa.
Maafisa hao waliovalia sare wanaoekana wakiiba, kama ilivyopewa na video ya CCTV iliyopeperushwa na NTV, Agosti 29.
Wanjiru anashikilia kuwa, mgogoro kati yake na polisi ulianza baada ya kukataa kulipa KSh 1,000 kila mwezi wanazodai polisi ni za kutoa huduma za ulinzi usiku.
"Sitolipa wala kuwapa hongo yoyote. Wanataka KSh 1000 na nimelipa ada ya kuendesha biashara na kupewa leseni. ISitowapa hapa peni," aliapa Wanjiru.