Skip to main content

Gavana wa Machakos Alfred Mutua Azindua Kituo Cha Matibabu ya Saratani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 August 2019.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua Azindua Kituo Cha Matibabu ya Saratani

Kituo hicho kilizinduliwa mnamo Alhamisi, Agosti 29, 2019, katika hospitali ya Machakos Level V.

Kituo hicho kimejengwa na vifaa vya kisasa na kitaboresha matibabu ya wagonjwa wa saratani ambao watahudumiwa bila malipo.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua alifichua kwamba, kituo hicho ambacho kimejengwa na vifaa vya kisasa kitaboresha matibabu ya wagonjwa wa saratani ambao watahudumiwa bila malipo.

Kituo hicho ambacho kimejengwa katika hospitali ya Machakos Level Five kilipokea ufadhili kutoka kwa wahisani mbali mbali ikiwemo Wizara ya Afya, taasisi ya kitaifa ya saratani, Path, Bioventures for Global Health, hospitali kuu ya Kenyatta, Ampath na Lions Club.

Wakazi wa Machakos ambao wamesajiliwa chini ya mwavuli wa Universal Health Coverage (UHC) watakuwa miongoni mwa wale ambao watapokea matibabu ya saratani bila malipo.

Kituo hicho pia kimejengwa ili kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa na familia zao.

Uzinduzi wa kituo hicho kumewapa matumaini Wakenya kwa jumla, kufuatia maafa ambayo yamesababishwa na saratani hususan kwa watu mashuhuri nchini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →