This archive report was first published on 29 August 2019.
Mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa washukiwa saba waliohusishwa na ajali ya boda boda eneo la Kutus-Kianyaga, Agosti 25, 2019, alizua kihoja mahakamani siku ya Jumatano, Agosti 28, 2019.
Alipofika mahakamani, alianza kuimba na kuzungumza kwa ndimi, kufanya Hakimu Mkuu Ann Katheria kuiamuru kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kurejeshwa kortini.
Washukiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Gichugu, ambapo walituhumiwa kwa kuzua rabsha na uharibifu wa mali.
Washukiwa hao walikisiwa kuchoma gari la polisi ambalo lilimgonga muhudumu wa boda boda kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika eneo la Rwambiti katika barabara ya Kutus-Kianyaga, siku ya Jumapili, Agosti 25, 2019.
Naibu OCPD wa Gichugu, Alfred Ng’eno, alisema mhudumu huyo wa boda boda alifariki papo hapo, huku abiria mmoja akifariki katika Hospitali ya Kerugoya baada ya kukumbana na majeraha, mwathiriwa wa tatu akiendelea kupokea matibabu.