This archive report was first published on 28 August 2019.
Seneta Mithika Linturi alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na mke wake Marianne Kitany, kwa hivyo aliamua kuomba talaka.
Kitany alisema aligundua kuwa Linturi alikuwa na vipusa nje ya ndoa ambao walikuwa wakikata kiu yake ya mapenzi.
Alisema pia kuwa aligundua kuna akina dada ambao walikuwa wakitumia Linturi picha na vidio wakiwa uchi na hivyo akaamua watamatishe ndoa yao.
Kitany alisema alipewa miraa iliyokuwa imefungwa na kufanana na kiungo cha mwanamume wakati wa sherehe ya kuoana kwao.
Alisema Linturi alimwarifu kuwa hiyo ilikuwa saini ya ndoa yao.
Kitany alizungumza kwenye mahakama ya Milimani mbele ya jaji Peter Ngare na kuonyesha picha na vidio za kuonyesha kuwa wawili hao walikuwa wameona na kuishi kama mke na mume.
Alisema wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwake, Linturi anaskika akimuimbia 'Happy Birthday' na kusema 'I love you'.