This archive report was first published on 28 August 2019.
Magazeti ya Jumatano, Agosti 26 yameangazia taarifa kuhusu mvutano wa mamlaka kati ya Naibu Rais William Ruto na Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Raphael Tuju.
Mvutano huo unafuatia Tuju kukanusha orodha ya wagombeaji wa kiti cha Kibra kutoka chama hicho kiliocho wasilishwa kwa IEBC.
Naibu Rais William Ruto pamoja na bodi ya uchaguzi wa chama hicho walikuwa wamewasilisha orodha ya wagombeaji watano kwa IEBC, ikijumuisha mwanasoka McDonald Mariga.
Orda nyingine iliyoshinikizwa na Tuju inakisiwa kuwasilisha majina ya Doreen Wasike au Maurice Peter Kinyanjui kama wagombeaji.
Uchaguzi mdogo wa Kibra ambao umeratibiwa kuandaliwa mwezi Novemba 7 utashirikisha chama hicho tawala na ile ya Upinzani ya ODM katika kinyang'anyiro cha kwanza cha kisiasa tangu kuwa na maafikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Polisi walimkamata mwanabiashara tajiri wa Mombasa Ali Punjani siku ya Jumatatu, Agosti 26 baada ya kukosa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JKIA ambapo walikuwa wamekita kambi kusubiri kumkamata.
Maafisa hao walitambua kuwa jina la Punjani lilikuwa limeorodheshwa kwenye orodha ya wasafiri waliokuwa wanatazamiwa kuabiri ndege kutoka JKIA kuelekea Mombasa.
Polisi walimkamata mkewe mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni raia wa Nepal pamoja na washukiwa wengine wawili mnamo Jumanne, Agosti 13.
Msomaji wa Serikali Cyrus Oguna alisema familia wanaoishi mitaani hawata shirikishwa kwenye zoezi linaloendelea la sensa.
Source: Tuko Newspaper