This archive report was first published on 26 August 2019.
Polisi wamekamatwa watu wawili Chepalungu, Bomet baada ya kukataa kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa.
Wakati zoezi la kuhesabu watu lililoanza rasmi Jumamosi, Agosti 24, likiendelea visa vya kihuni vinaendelea kushuhudiwa maeneo mbalimbali dhidi ya maafisa wa sensa.
Maafisa wa polisi walimkabili haraka na kumkamata mwanamume huyo wa umri wa makamo kwa kukataa kushiriki zoezi la sensa na anazuiliwa.
Atafikishwa kortini na kushtakiwa kwa kosa la kukataa kuhesabiwa, alisema Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Chepalungu Nelson Masaai.
Maafisa wake walitumia nguvu kuingia katika boma la mwanamume huyo eneo la Kipsuter kwa kuwa alikuwa amekataa kuwafungulia lango.
Alisema kuwa zoezi hilo liliendelea shwari baada ya tukio hilo.
Alisema pia, polisi wanamsaka mwanamume kutka kijiji cha Kapletundo aliyekataa kuorodheshwa Alhamisi, Agosti 22 kabla ya zoezi hilo kuanza rasmi.
Atakamatwa na kushtakiwa kwa kuwa alikuwa na masuala binafsi kuhusu zoezi hilo baada ya mwanawe kukosa kufalu kuwa mmoja wa maafisa wa sensa, alisema Kamishna wa Kaunti ya Bomet Geoffrey Omondi.