This archive report was first published on 26 August 2019.
Makosa ya Mazoea Katika Kiswahili ¶
Leo, tutakapofika, tutazidi kuangaza makosa ya mazoea katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Katika makala yetu ambayo yamepita, tumekuwa tukiweka mwanga katika Kiswahili na kuinyoosha lugha. Published on August 26, 2019
Leo, tutazidi kuona na kunyoosha palipo na utata. Picha: UGC
Makosa: Chakula Chenye Tulikula Kilikuwa Hakijaiva ¶
Neno "chakula" limetumika visivyo. Sahihi: Chakula ambacho tulikula kilikuwa hakijaiva au Chakula tulichokula kilikuwa hakijaiva.
Makosa: Viongozi Wenye Tulichagua Ni Fisadi ¶
Sahihi: Viongozi ambao tulichagua ni fisadi au Viongozi tuliowachagua ni fisadi.
Makosa: Gari Lenye Amenunua Ni Nzuri Sana ¶
Sahihi: Gari ambalo amenunua ni zuri sana au Gari alililonunua ni zuri sana.
Makosa: Hakuna Binadamu Hapendi Maendeleo ¶
Sahihi: Hakuna binadamu asiyependa maendeleo.
Makosa: Wanafunzi Wenye Walikalia Mtihani Mwaka Jana Walipasi Vizuri ¶
Sahihi: Wanafunzi ambao walifanya mtihani mwaka jana walipasi vizuri au Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka jana walipasi vizuri.
Makosa: Mtoto Yule Ni Mrefu Kuwaliko Wazazi Wake ¶
Sahihi: Mtoto yule ni mrefu kuliko wazazi wake.
Makosa: Mtoto Yule Ni Mnene Kumliko Wake ¶
Sahihi: Mtoto yule ni mnene kuliko wake.
Wakati unapotumia "o" rejeshi huwezi kutumia pamoja na kirejeshi amba. Mfano zaidi ya makosa haya ni;
Makosa: Mtu Ambaye Aliyekuja Alikuwa Mgeni Wetu
Sahihi: Mtu ambaye alikuja alikuwa mgeni wetu au Mtu aliyekuja alikuwa mgeni wetu.
Kumbuka Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie.
Makala haya yameandikwa na Sakwa Titus mwalimu, mhakiki na mwandishi.