Skip to main content

Afisa wa Kuhesabu Watu Atatiza Shughuli baada ya Kulewa Chakari na Kuanguka Mtoni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 August 2019.

Shughuli za kuhesabu watu zilikuwa zimeanza Jumamosi Agosti 24, na serikali ilihakikisha Wakenya usalama wote.

Shughuli hiyo ilikuwa ikikabiliwa na hitilafu huko West Pokot baada ya vifa kuibiwa.

Na huko Kakamega, afisa wa kuhesabu watu alibugia kileo kuzidi na kuanguka mtoni.

Alilewa kiasi cha kwamba alianguka kwenye mto akiwa na kifaa chenye nambari 3708020301015EA ambacho kilipata maji.

Aliokolewa na majirani na kupelekwa hadi katika kituo cha polisi.

Alikamatwa na kuzuiliwa huku akisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu Agosti 26.

Shughuli za kuhesabu watu huko West Pokot huenda zikatatizwa baada ya vifaa vya maafisa wa kuhesabu watu kuibiwa.

Wafanyikazi wa shughuli za kuhesabu watu walivunja afisi iliyokuwa na vifaa vya kuwahesabu watu na kuviiba huko Kapenguria, Kaunti ya West Pokot.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →