Skip to main content

Mkenya Ahukumiwa Miaka 15 Jela Kwa Kuiba Mapambo ya Thamani ya KSh 55M

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 21 August 2019.

Mapema mwezi Machi 11, 2019, Victor Okumu, 38, alikuwa amekabidhiwa hukumu ya miaka 13 jela kwa kuingia katika nyumba ya mwanamke mmoja na kumwibia. Hata hivyo, baada ya kuachiliwa huru mnamo Machi 20, 2014, Okumu alichagua kukaa katika nchi hiyo.

Okumu alitekeleza wizi huo wa kimabavu mnamo Machi 11, 2019, katika duka la Bradleys The Jewellers, eneo la Northallerton, Yorkshire Kaskazini, Uingereza. Kulingana na ushahidi, aliruka kaunta akiwa amevalia kofia ya helmeti na msurupwenye.

Polisi hawajapata nusu ya mapambo aliyoiba Okumu kutoka kwenye duka, lakini alipokuwa akikabidhiwa hukumu, jaji alisema kuwa wizi alioufanya Okumu ulikuwa wa kupangwa muda mrefu kabla ya kutekeleza.

Okumu atakaa jela miaka 15 na mwaka mwingine mmoja kwa kuiba mapambo akitumia nguvu. Kwa mujibu wa ripoti ya YorkExpress, ambayo TUKO.co.ke imeisoma, majaji wa korti ya rufaa walikuwa wamependekeza Okumu kutimuliwa miaka kumi iliyopita akikamilisha kifungo chake cha miaka 13 jela.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →