Skip to main content

Wasiomwamini Mungu Wasema Miujiza ya Nabii Owuor ni Porojo

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 19 August 2019.

Wasiomwamini Mungu Wasema Miujiza ya Nabii Owuor ni Porojo

Wasiomwamini Mungu wa Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu miujiza inayotokea kwa Nabii Owuor, wakidai kuwa ni porojo ili kuwahadaa washirika.

Wasiomwamini Mungu wa Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu miujiza inayotokea kwa Nabii Owuor, wakidai kuwa ni porojo ili kuwahadaa washirika. Mwenyekiti wa muungano huo, Harrison Mumia, alisema Nabii Owuor ni mmoja wa wale ambao wanaeneza miujiza ya uongo ili kuwahadaa washirika.

"Tunaelewa kuwa kanisa linaaminika na washirika kuwa nyumba ya Mungu na mahali patakatifu ambapo miujiza hufanyika na pia kupata utulivu kutokana na shida za kimaisha. Wengi hutarajia matatizo yao ya kifedha yatafika mwisho wakiwaskiza wahubiri," alisema Mumia.

Wasiomwamini Mungu wa Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu miujiza inayotokea kwa Nabii Owuor, wakidai kuwa ni porojo ili kuwahadaa washirika. Muungano huo unasema kuwa baadhi ya wahubiri wanachua nafasi ya washirika wao kuwa katika hali hii ya kutarajia muujiza na hivyo kuwahadaa kwa njia kali.

"Hata hivyo, tunaona kuwa baadhi ya wahubiri akiwemo Nabii Owuor wamekuwa wakichukua nafasi hiyo na kuigiza miujiza ili kuwavutia huku wakifanya kana kwamba ya miujiza ya Mungu. Hili si lingine mbali kuwahadaa washirika wao," aliongeza.

Hayo yalijiri wakati ambapo Nabii Owuor alikuwa akifanya mkutano mkubwa kwenye eneo la Menengai Grounds mjini Nakuru. Washirika wa Owuor walifurika kwenye eneo hilo kuanzia Ijumaa Agosti 18.

Be the first to react

Follow the next update

Build Nyakundi Report with us

Join the official channels for story updates, video drops, and alerts from the newsroom. Call 0710 280 973.

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →