Skip to main content

Takriban Wabunge 60 wanaugua Saratani, Gavana Sonko anasema

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 July 2019.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema kuwa takriban wabunge 60 wanaugua saratani, kwa mujibu wa ripoti zake.

Alisema hii wakati wa kuomboleza mbunge Joyce Laboso ambaye alifariki dunia Jumatatu, Julai 29, baada ya kuugua saratani.

Laboso alikuwa Gavana wa Kaunti ya Bomet.

Alisema ugonjwa huo sasa ni jinamizi na serikali inafaa itafute mbinu za kukabili.

Alisema hii wakati wa kuwataka viongozi wajitokeze ili waweke mikakati ya jinsi ambavyo watapigana na janga hilo.

"Saratani ni ungonjwa ambao unakithiri sana, ripoti ambazo tunapata ni kuwa kuna wabunge sitini ambao wanaugua ugonjwa huu wa saratani na lazima tuketi chini kama viongozi na tupange jinsi tutakabiliana nao," Mike Sonko alisema.

Wabunge wengine wanaugua saratani ni Francis Waititu, ambaye alisema aliweza kupokea matibabu na kwa sasa ana nafuu ya kutosha kuchapa kazi.

Waititu alisema, "Watu wengi sana wanaugua Saratani. Hakuna mtu anataka kuongea kutokana na unyanyapaa unaohusishwa na saratani. Nchini India, nilikutana na mamia ya wanaougua saratani kutoka Kenya," Mbunge huyo alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →