Skip to main content

Pasta Lucy Natasha Aondoa Mwaka Mwingine, Sherehe Yake Iliyokuwa ya Kukata na Shoka

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 July 2019.

Mwanzilishi wa kanisa la Prophetic Latter Glory Ministries International, Pasta Lucy Natasha, aliongeza mwaka mwingine katika umri wake siku ya Jumatano, Julai 24, 2019.

Sherehe yake ya siku yake ya kuzaliwa ilikuwa ya kukata na shoka, na ilihudhuriwa na jamaa zake.

Alijiandalia sherehe hiyo kwa wale awapendao mazuri, na kutokea kwa mamake, msaidizi wake na kanisa lake kwa jumla, alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Sherehe hiyo ilikuwa na kielelezo cha rangi nyeupe na nyekundu, iliandaliwa na wadogo wake pamoja na msaidizi wake ambao aliwashukuru kupitia kwa mtandao wake wa Instagram.

Alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Natasha alitoa ujumbe wa heri kwa wafuasi wake, na kwa picha alizoanika ni ishara tosha kuwa mtumishi huyo wa Mungu pamoja na wafuasi wake walitumia pesa nyingi katika kuandaa sherehe hiyo.

Alipokuwa akiandika kuhusu sherehe hiyo, Natasha alisema, ''Siku ya kuzaliwa yenye furaha. Nawashukuru wadogo wangu Joseph Shafique na Shiphrah Murathe pamoja na msaidizi wangu Princess Irene kwa kuandaa chajio huku tukimshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake. Mkono wa Mungu watufanya washindi kila siku,''.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →