This archive report was first published on 29 July 2019.
Gavana wa Bomet Joyce Laboso ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, Jumatatu Julai 28, 2019.
Laboso alipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi ambapo aliripotiwa kuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa majuma wawili.
Alirejea humu nchini Julai 14, 2019, kutoka India ambapo alikuwa akipokea matibabu.
Taarifa za kifo chake zinajiri saa chache baada ya serikali ya kaunti ya Bomet kutoa taarifa kuwa gavana huyo alikuwa anaendelea kupata nafuu.