This archive report was first published on 27 July 2019.
Julai 25, 2019, ilikuwa siku ya kudanganywa kwa wabunge wa jimbo la Ondo nchini Nigeria wakati nyoka wa ajabu alikimbia bungeni na kuwafanya wakimbilia usalama wao.
Wabunge wengi waliingiwa na uoga na walilazimika kusitisha vikao vyao na hatimaye kuahirishwa.
Olugbenga Omole, semaaji wa wabunge hao, alisema kwamba tulipokuwa tukikaribia kuingia bungeni, nyoka mkubwa alikimbia nje ya bunge na kutufanya kuingiwa na uoga na kusababisha vikao kuahirishwa.
Omole alisema, "Kila mtu alikimbia".
Shughuli katika bunge hilo kwa sasa zimesimamishwa hadi litakapokarabatiwa na mashimo yote yanayoweza kupitisha wanyama mfano wa nyoka kuzibwa.
Wabunge walitaja kuwa tukio hilo linatokea kwa sababu ya hali mbaya ya jengo la bunge ambalo linakosa pesa la kulikarabati.
Hamna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho, lakini mfanyakazi wa bunge alimfukuza nyoka huyo na kumpiga hadi kufa.
Omole alisema, "Bunge sio salama na tumeamua kuahirisha vikao kwa muda ili lifanyiwe ukarabati unaofaa na kulifanya saama kwetu".