This archive report was first published on 25 July 2019.
Profesa Anyang Nyong'o, Gavana wa Kisumu, na dadake Risper Nyogoy wamejipata taabani baada ya kesi ya urithi inayowakabili.
Wawili hao wamejipata taabani kutokana na kesi ya urithi inayowakabili huku wakidaiwa kupuuza uamuzi wa mahakama.
Wakipatikana na hatia, wawili hao huenda wakafungwa kifungo cha mwezi mzima gerezani.
Wawili hao walikuwa wametakiwa na mahakama kulipa shilingi 400,000 kila mmoja kwa kukosa kufika kwenye kesi yao.
Uamuzi huo ulitolewa na jaji Thripsisa Cherere, ambaye alisema wawili hao walikuwa wameonyesha wanaidharau mahakama sana.
Wakati wa kesi hiyo, jaji huyo alikuwa amewataka wawili hao kutoa hesabu kuhusu mali yaliyokuwa yanamilikiwa na baba yao.
Wakati wa kesi hiyo, jaji huyo alikuwa amewataka wawili hao kutoa hesabu kuhusu mali yaliyokuwa yanamilikiwa na baba yao.