Skip to main content

Jamaa amposa mpenziwe wakati wa hafla ya kuhitimu kwake katika chuo kikuu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 July 2019.

Agne Banuskeviciute, mwanadada wa umri wa miaka 25, aliposwa na mpenziwe wakati wa hafla ya kufuzu kwake katika Chuo Kikuu cha Essex, Uingereza.

Agne alikuwa na hisia mseto kwa kuwa alijua kulikuwepo na jambo, lakini hakujua lilikuwa ni lipi.

Alisema, "Nakumbuka nikiwa jukwaani. Nilikuwa na hisia mseto kwa kuwa nilijua kulikuwepo na jambo."

Aliongeza, "Kisha kila kitu kilitendeka kwa haraka kwani ilinichukua muda kabla nibaini kilichokuwa kikifanyika."

Agne aliposwa na mpenziwe, alikuwa na furaha mara dufu, na alifichua jinsi alivyoingiwa na hofu kumwona mpenziwe akielekea jukwaani.

Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miaka tisa, na wamekuwa marafiki tangu wakiwa shule ya upili.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →