Skip to main content

Boris Johnson Chaguliwa Kuwa Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 July 2019.

Uchaguzi uliofanywa kwa muda wa majuma saba ulikuwa na matokeo muhimu kwa siasa za Uingereza, na Boris Johnson akashinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656.

Boris Johnson, ambaye aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Conservative Jumanne Julai 23, atapokea wadhifa huo kutoka kwa Waziri Mkuu anayeondoka Theresa May hapo kesho Jumatano, Julai 24.

Boris Johnson ameahidi kuiunganisha nchi ambayo kwa sasa inakumbwa na mzozo wa kisiasa, na viongozi kadhaa akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump na Theresa May tayari wamempongeza Boris kwa ushindi huo.

Habari hii inatokana na gazeti la The Guardian nchini Uingereza.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →