Skip to main content

Wafuasi wa Ruto wachemka baada ya Waziri Rotich kutiwa mbaroni ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 22 July 2019.

Wafuasi wa Naibu Rais William Ruto wamekosoa vikali uamuzi wa kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Haji kuagiza kukamwa kwa Waziri Henry Rotich baada ya kuhusishwa kwenye wizi wa mamilioni ya pesa ya miradi ya mabwawa Arror na Kimwarer.

Seneta Kipchumba Murkomen, Aaron Cheruiyot, na mbunge Oscar Sudi wamekosa uamuzi huo, kwa kusema kuwa ni njama tu ya kisiasa na wala si vita dhidi ya ufisadi.

Seneta Murkomen alisema, "Nimeangalia mashtaka na ninataka kuwaambia huu wote ni mpango fulani," huku seneta Cheruiyot akisema kuwa kuna miradi mingine ambayo pia imekwama na anashangaa ni vipi DCI waliamua kuangazia Kimwarer na Arror pekee.

Mbunge wa Kapseret Oscah Sudi alisema kukamatwa kwa Rotich pamoja na maafisa wengine wanaohusishwa na ufisadi kwenye miradi ya mabwawa hayo ni vita dhidi ya jamii ya Wakalenjin pamoja na Naibu Rais William Ruto.

Rotich alikamatwa Jumatatu, Julai 22, baada ya kuhusishwa kwenye wizi wa mamilioni ya pesa ya miradi ya mabwawa Arror na Kimwarer.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →