Skip to main content

Moses Kuria Rejects Uhuru's Support for Pre-2022 Constitutional Referendum

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 21 July 2019.

Published on July 21, 2019, Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amesema taifa halifai kushiriki kura ya mageuzi ya katiba kabla ya mwaka wa 2022.

Mbunge huyo amesema atakabiliana kisiasa na watakaounga mkono mageuzi ya kabla ya 2022, akiwemo Rais Uhuru Kenyatta iwapo atakuwa mmoja wa wale watakaokubali mageuzi yafanywa kabla ya wakati huo.

Alisema mageuzi yoyote ya sasa yafanyike ndani ya bunge, na kwa hivyo, mageuzi yafanywa kabla ya 2022 yatakuwa ya kisiasa tu.

“Siwezi kuunga mkono referenda iandaliwe kabla ya 2022. Naunga mkono hatua ya katiba kufanyiwa marekebisho kadhaa, lakini yale yanawezekana kufanywa na bunge yafanywe sasa, kisha wakati wa Uchaguzi Mkuu 2022 tupige kura ya maamuzi,” alisema Kuria.

Aliongeza, “Hatutasimamisha taifa ili kufanya referenda. Haitafanyika hivyo.”

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →