Skip to main content

Mwanasiasa Francis Mureithi awaonya wakazi wa Mlima Kenya dhidi ya kumsaliti William Ruto

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 July 2019.

Naibu Rais William Ruto amekuwa kwenye kipaumbele kwa kipindi kisicho cha muda, na wakazi wa Mlima Kenya wamekuwa wakimsaidia kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, mwanasiasa Francis Mureithi amewaonya wakazi wa eneo hilo dhidi ya kumsaliti Ruto, kwa kusema kwamba haitakuwa haki ikiwa viongozi na wakazi wa Mlima Kenya watamgeuka Ruto hata baada yake kuwaunga mkono kwa hatamu mbili za uongozi.

Francis Mureithi alionya dhidi ya kumhadaa William Ruto jinsi ambavyo waliwafanyia Raila na Kalonzo. Picha: Francis Mureithi/ Facebook

Alisema hivi katika mafunzo yake ya Biblia mnamo Ijumaa, Julai 19, ambapo alitumia kisa cha Onan kwa ajili ya kuonyesha madhara yanayoweza kutokea ikiwa wakazi wa Mlima Kenya watakuwa na roho chafu na kutenda kinyume na ahadi yake.

"Hata Biblia inasema, mutaanza na Yerusalemu, mwende Samaria kisha Judea. Samaria yetu ni Ruto mnajua ni nani alitusaidia na pia tuliafiki makubaliano mjini Nakuru, ambapo hapo ndipo Mlima Sinai," alisema.

Aliongeza, "Tuliagana iwapo angetusaidia kupata ushindi, tungemsaidia pia." Matamshi hayo yalionekana kuufurahisha umati huo ambao ulianza kushangilia hususan baada ya kufichua adhabu itakayowafika wakaazi baada ya kuilinganisha na hadithi yake Onan.

Source: Tuko.co.ke

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →