Skip to main content

Elgeyo Marakwet: Kamishna Natembeya Ameuambia Machifu Kuacha Uzembe Kazini

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 July 2019.

Julai 17, 2019, Kamishna wa Kaunti ya Bonde la Ufa George Natembeya alitoa wito kwa machifu wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet kujitahidi zaidi katika kushughulikia ulemavu wa kijamii wa wezi wa mifugo eneo hilo.

Aliwataka machifu hao kuacha uzembe kazini ili kufanikiwa katika vita dhidi ya wezi wa mifugo, na kuwahimiza kukabiliana vikali na wahalifu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi wa eneo hilo kwa kuendeleza visa vya wizi wa mifugo.

Aliwashutumu maafisa hao hasa wa usalama wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet kwa uzembe na kuwaonya kuhusu adhabu kali dhidi ya watakaokosa kutambua wezi wa mifugo.

"Haiwezekani kwa naibu chifu kutofahamu hawa watu ambao wamekuwa wakitembea na bunduki na kuwatisha wakazi wa hapa," alisema Natembeya.

Aliwaonya pia wahalifu na wezi wa mifugo kusalimisha silaha zao na kuwaonya kuwa serikali itatumia njia zinazofaa ikiwamo nguvu katika kutafuta bunduki zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

"Nawaonya...tuthakikisha tunamaliza wizi wote wa mifugo. Tuko tayari kuwalipua kwa mabomu," alisema Natembeya.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →