MITAMBO: Kifaa cha kukama ng'ombe chawafaa wenye mifugo wengi ¶
Na Richard Maosi
Wakulima wenye mifugo wengi wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata tija zaidi kwa gharama nafuu kwa kutumia kifaa cha kukama ng'ombe.
“Ishara tosha kuwa atafanikiwa kuendesha kilimo kwa njia ya kisasa na kwa wakati huo kupata tija zaidi kwa gharama nafuu,” anasema mtaalam wa mifugo na bidhaa zinazotokana na maziwa kutoka Chuo Kikuu Cha Egerton Nakuru, Gabriel Kwendo.
Matumizi ya kifaa cha kukama ng'ombe hupunguza uwezekano wa mkamaji kuathiri maziwa au kiwele cha mifugo moja kwa moja.
“Baada ya kuwasha stima kifaa huanza kukanda zile chuchu na hatimaye kufyonza maziwa, labda kwa dakika kumi tu na shughuli huwa imekamilika,” anaeleza.
Wakulima wadogo mashambani bado wanapendelea kutumia mikono yao kukama, wenzao katika sekta ya ufugaji ng'ombe wa maziwa kwa madhumuni ya kibiashara wanatumia mitambo.
“Kwa sababu mimi ni mfugaji wa ng'ombe wengi, ninatumia kifaa cha milking machine, kwani kina uwezo wa kukama maziwa mengi kwa urahisi bila kuumiza chuchu za ng'ombe,” anaongeza.