Wawaniaji waeleze jinsi watakavyonasua Wakenya kutoka lindi la mahangaiko

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, unatia moyo wanachama wa vyama vya siasa kuelezea jinsi watakavyoanzisha mikakati ya kuboresha maisha ya Wakenya.

Wanachama hawa wanaelezea kwamba msingi wa uchumi wetu ulikuwa umeharibika kitambo hata kabla ya janga la corona, na kwamba viongozi ambao watachukua hatamu baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022, na wanaosaka kura wakati huu, wafaa kumakinika zaidi na kuelekezea mikakati mipya watakaotumia kuboresha maisha ya Wakenya.

Wagombeaji wakuu wa urais; Naibu Rais William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, waelezee kwa uwazi jinsi mifumo yao ya kiuchumi itaondoa Wakenya kutoka lindi la mahangaiko.

Naibu Rais William Ruto aeleze jinsi mfumo wake wa kukuza uchumi kutoka ngazi ya mashinani, maarufu kama "bottom-up", utatekelezwa kwa manufaa ya walalahoi.

Naibu Rais William Ruto aeleze jinsi, fedha hizo zitasimamiwa ili kuzuia uwezekano wa kuibiwa na maafisa wa serikali walafi namna ambavyo fedha za Hazina ya Uwezo ziliporwa.

Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga aelezee Wakenya jinsi utawala wake utatambua familia masikini na ambazo zitafaidi kutokana na ruzuku ya Sh6,000 kila mwezi.

Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga pia aelezee Wakenya mbinu mpya atakazotumia kufufua viwanda vikubwa vilivyosambaratika kama vile kampuni ya kutengeneza sukari za Mumias, Nzoia, Miwani, Sony, Muhoroni, Chemilil na kampuni ya Ramisi iliyoko Pwani.

Next read

Former Mandera Police Officer Convicted for Assaulting Two Civilians Now Serving 16-Year Sentence at Kamiti Maximum Prison

16 October 2026 · 3 min read

Convicted former Mandera East Police Station officer Abdihakim Abdi Saman serving his sentence at Kamiti Maximum Security Prison.