Skip to main content

Daktari wa Mifugo Asema Upekuzi wa Dennis Okari Uliitiwa Chumvi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 16 July 2019.

Upekuzi wa Dennis Okari wa Red Alert ulikuwa na matokeo makubwa, lakini daktari Kenneth Wameyo amesema ulitiwa chumvi na kuwa hakuna uwezekano wa dawa hiyo kusababisha saratani.

Wameyo, daktari wa mifugo, alisema hii Jumapili, Julai 14, 2019, baada ya Dennis Okari kutoa taarifa ambayo ilisema dawa inayotumiwa kwenye maduka ya nyama ni hatari na inaweza kusababisha saratani.

Okari alisema kuwa dawa hiyo ni aina ya sodium metabisulfite, ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa saratani, lakini Wameyo alisema hili si kweli na kuwa dawa hiyo hutumiwa kurefusha maisha ya vyakula.

Wameyo alisema kuwa ingawa maduka ya nyama yanatumia dawa hiyo kurefusha maisha ya nyakula wanayouza, taarifa hiyo iliwasilishwa kwa njia ambayo ilitiwa chumvi mno.

Aliendelea kukoa wataalamu waliohojiwa na Okari kwenye taarifa yake akisema kuwa si magwiji katika maswala ya lishe na hivyo maoni yao hayawezi kuchukuliwa kwa uzito.

Wameyo alisema kuwa ingawa ni muhimu kujua kuwa maduka ya nyama yanatumia dawa hiyo, taarifa hiyo iliwasilishwa kwa njia ambayo ilitiwa chumvi mno na kuwa hakuna uwezekano wa dawa hiyo kusababisha saratani.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →