Waziri wa Elimu, George Magoha, amesema kila mwanafunzi ajiunge na Kidato cha Kwanza, na hivyo kuhepa wazazi kuwajibika kwa kulipa karo.
Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Machakos, Kahi Indimuli, ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao wanajiunga na Kidato cha Kwanza walipe karo na wakome kutumia kauli ya Waziri wa Elimu, George Magoha.
Aliwataka wazazi wanaokosa kulipa karo wawe na sababu ya kutofanya hivyo.
"Katika kutekeleza sera za serikali, lazima pia tupate msimamo ifaayo kwa nini mzazi hawezi kutimiza wajibu fulani. Tunataka wazazi waeleze ni kwa nini hawawezi kulipa karo na wala si kutumia kauli ya waziri kama kisingizio. Hilo halikubaliki," akasema Bw Indimuli.