Profesa Magoha asinyamaze walimu wakuu wakiwaongezea wazazi gharama zaidi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Profesa George Magoha, Waziri wa Elimu, amesahau kwamba aliwaagiza walimu wakuu kutowaongezea wazazi gharama zaidi wakati wa kuwataka wawanunulie vitu vingi "visivyo na umuhimu mkubwa" kwa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.

Alitoa uamuzi huo mnamo Aprili 11, 2022, wakati wa kuzindua rasmi shughuli ya uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza katika Taasisi ya Kuandaa Mitaala Nchini (KICD) huko Nairobi.

Profesa Magoha alisema kwamba mwenendo huu wa walimu wakuu, haswa wa shule za upili za mabweni, kuwataka wazazi wawanulie vitu vingi huenda ukachangia baadhi yao kushindwa kumudu gharama hiyo.

Alisema kwamba matokeo yake ni kwamba watoto wengi watakosa kujiunga na shule za upili, hali inayoenda kinyume na sera ya serikali ya kuhakikisha kuwa watoto wote waliofanya mtihani wa KCPE wanawezeshwa kuendelea na masomo.

Next read

Fresh Documents Complicate Battle Over Ukombozi Name as Sifuna, Natembeya and Azimio Camps Collide

21 September 2026 · 6 min read

Fresh documents reveal how The Ukombozi Alliance was reserved in July while an earlier Ukombozi People’s Party registration had not been...