This archive report was first published on 16 July 2019.
Julai 15, 2019 - Mwanamke wa miaka 39 alipoteza sikio lake na sehemu ya mdomo wa chini baada ya mumewe kumuua kwa kupeana mboga.
Jackline Kerubo alisema mumewe Pascal Omusungu aliudhika baada ya jirani wao kufika nyumbani na kuomba mboga.
Alisema mumewe alipokasirika, jirani aliondoka bila kupewa mboga hizo.
Alisema kabla hata jirani afunge lango baada ya kutoka, Kerubo alisema aliskia kofi kali usoni ambalo lilimuangusha na kumfanya apoteze fahamu.
Aliongea na vyombo vya habari Jumatatu, Julai 15, mama huyo alilia kwa maumivu aliyokuwa nayo huku akiwa na shida kuzungumza kutokana na ukose wa eneo la mdomo wa chini.
Alisema isipokuwa ni mwanawe alimvamia babake kwa kifaa butu na kumfanya amamkie, angemjeruhi zaidi kwenye viungu vingine mwilini.
Visa vya vita baina ya wapenzi nchini Kenya vinazidi kushuhudiwa licha ya juhudi za kuvikabili.