Waziri Magoha Ameomba Majaji Watupilie Mbali Kesi Inayopinga Mfumo Mpya wa Elimu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Waziri wa Elimu Prof George Magoha ameomba majaji watatu wa Mahakama Kuu kuondoa kesi inayopinga mfumo mpya wa elimu (CBC) baada ya mzazi Esther Ang'awa kuomba kuiondoa.

Prof Magoha alipiga hatua hii kupitia kwa wakili Philip Murgor, akisema kuwa kesi hiyo inaathiri mamilioni ya wanafunzi kote nchini.

Bi Ang'awa alisema kuwa tangu awasilishe kesi hiyo ya kupinga CBC, asasi mbalimbali za serikali zimekuwa zikimwandama.

“Sitaki kuendelea na kesi hii kwa vile naandamwa. Nahofia elimu ya mtoto wangu itaborongwa na washika dau endapo nitaendelea na kesi,” alisema Bi Ang'awa katika ombi kortini.

Bi Ang'awa alisema kuwa mfumo wa CBC ni ghali na unawalimbikizia mzigo mzito wanafunzi na wazazi.

Wakili Nelson Havi, ambaye alipewa kujihusisha na kesi hiyo, alisema kuwa kesi hiyo ina umuhimu wa kitaifa na inazua masuala mazito ya kikatiba.

“Kesi hii iko na umuhimu wa kitaifa kutokana na athari zake. Naomba nikubaliwe kuendelea nayo kama wakili niliyeelezwa athari za mtaala huu mpya unaokandamiza haki za mamilioni ya wanafunzi,” alisema Bw Havi.

Wakili Philip Murgor alipiga marufuku ombi la Bw Havi, akisema kuwa hana uhusiano wowote na mlalamishi.

Majaji hao walitenga Juni 9, 2022 kuamua ikiwa ama watamruhusu Bw Havi kuendelea na kesi hiyo au wataifutilia mbali.

Next read

Fresh Documents Complicate Battle Over Ukombozi Name as Sifuna, Natembeya and Azimio Camps Collide

21 September 2026 · 6 min read

Fresh documents reveal how The Ukombozi Alliance was reserved in July while an earlier Ukombozi People’s Party registration had not been...