Skip to main content

Gavana Alfred Mutua aandalia mkewe sherehe ya kukata na shoka baada ya kuhitimu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 15 July 2019.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua alimtangaza mkewe Lilian Ng'anga kufuzu na kuhitimu shahada ya Uzamili katika Usimamizi na Tathimini ya Mradi.

Alfred Mutua alimtangaza mkewe Lilian Ng'anga kufuzu na kuhitimu shahada ya Uzamili katika Usimamizi na Tathimini ya Mradi mnamo Jumamosi, Julai 13, 2019.

Sherehe hiyo ilikuwa na rangi nyeupe na zambarau na ilionekana kugharimu pesa nyingi kulingana na picha ambazo Lilian aliweka katika mtandao wake wa Instagram.

Alfred Mutua alisambaza picha za mke wake wakiwa pamoja huku mkewe akiwa amevalia kanzu ya kuhitimu na kumumiminia sifa tele.

''Hongera Lillyanne Nganga kwa kufuzu tena. Miaka iliyopita ulikuwa wa kwanza katika shahada yako yako ya kwanza. Leo ulikuwa wa kwanza katika darasa lako la shahada ya Uzamili ya Sayansi katika chuo kikuu cha JKUAT. Ulikesha usuku mzima ukisoma na sasa imekulipa. Ninajivunia kwako mpenzi wangu,'' alisema gavana huyo.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa familia hiyo na pia wanafamilia, pamoja na baadhi ya wanasiasa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →