IEBC: Wapigakura Wafu 250,000 Kutupwa Taifa Leo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

IEBC: Wapigakura Wafu 250,000 Kutupwa Taifa Leo

IEBC inasema kuwa kuna wapigakura wafu 250,000 kwenye sajili yao, na kwamba itakuwa vigumu kuondoa majina yao kwenye sajili rasmi.

Kamishna wa IEBC, Justus Nyang'aya, alisema jana kuwa itakuwa vigumu kuondoa wapigakura wote wafu katika sajili hiyo.

"Tumepokea karibu majina 250,000 kutoka kwa idara inayosajili vifo. Ukweli ni kuwa tutajitahidi sana kuyaondoa majina yao kwenye sajili rasmi lakini si wote kwa sababu watu hufa kila siku hata siku ya uchaguzi wenyewe bado kutakuwa na vifo," alisema Bw Nyang'aya.

IEBC inasema kuwa kuna wapigakura wapya 2.7 milioni walijsajiliwa kati ya 2018 na Februari 2022, na kwamba kati ya hao, wapigakura 1.519 milioni walisajiliwa kati ya Oktoba 2021 na Novemba 2021.

IEBC inatarajiwa itaanza kutoa mafunzo kwa maafisa wake watakaosimamia uchaguzi mkuu ujao, na kuwaajiri maafisa 530,000 kwa muda.

"Tulikuwa na vituo 44,300 vya upigaji kura mnamo 2017 lakini katika uchaguzi huu idadi hiyo itapanda hadi vituo 53,000," alisema Bw Nyang'aya.

Next read

Fresh Documents Complicate Battle Over Ukombozi Name as Sifuna, Natembeya and Azimio Camps Collide

21 September 2026 · 6 min read

Fresh documents reveal how The Ukombozi Alliance was reserved in July while an earlier Ukombozi People’s Party registration had not been...